Juzi jioni ilisemekana kuwa Kimwana mmoja akiwa katika gari lake kama wadau wa Blog mjuavyo foleni katika jiji letu,Naye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa wakielekea mitaa ya city centre inavumishwa kuwa ombaomba alifika katika dirisha la kimwana huyo na kuomba msaada baada ya kumpatia mkono wa kimwana huyo uliota manyoya,ili kuondoa dhahama hiyo ombaomba huyo alihitaji kupata busu na baada ya kumpa busu kimwana huyo alipotea ghafla.
Wadau wetu wa Blog ya habari walikwenda hadi kwa kamanda wa Polisi kanda maalum ya DSM na kutaka kujua ukweli wa jambo hilo kamanda alisema si kweli.
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa wakazi wa jijini kuvumisha mambo ambayo hayana ukweli wowote na kuleta maswali mengi miongoni mwa jamii.Kwa mfano:
I.Mwaka 1994 walivumisha habari ya mtu kugeuka chatu baada ya kuoga
maji yaliyotiwa dawa na kimwana wake kwa lengo la kudumisha majambozi na kwamba uvumi huo haukuishia hapo na kudai chatu huyo kapelekwa kituo cha polisi Buguruni na kujaza wakazi wengi kituoni hapo.
II.Uvumi wa kifo cha Mohammed Mpakanjia japo alifariki kweli mwaka 2009 baadae.
III.Uvumi wa kifo juu ya mzee wa Vijisenti.
IV.Maajabu ya mtu kufufuka makaburi ya kinondoni.
No comments:
Post a Comment