RAIS wa Kenya, Bw. Mwai Kibaki amewaagiza maofisa tisa waandamizi katika Serikali yake kauchia ngazi wakisubiri kuchunguzwa kwa kashfa za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Miongoni mwa maofisa hao ambao wametakiwa kuachia ngazi mmoja anahusishwa na hasara ya dola milioni 26 zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa mahindi.
Miongoni mwa maofisa hao ambao wametakiwa kuachia ngazi mmoja anahusishwa na hasara ya dola milioni 26 zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa mahindi.
Maofisa wengine waliosalia wanahusishwa na upotevu wa mamilioni ya dola katika Wizara ya Elimu.
Akitoa agizo hilo juzi Rais Kibaki aliwataka maofisa hao kuachia ofisa zao kwa muda wa miezi mitatu ili kuruhusu uchuinguzi kuhusu upoteaji wa fedha hizo za umma.
Orodha hiyo inawahusisha makatibu wakuu wanne.
Iliripotiwa kuwa muda mfupi kabla ya Rais Kibaki kutoa tamko hilo maofisa wawili waandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Raila Odinga walikwishatangaza kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kashfa ya mahidi ufanyike.
Hatua hiyo inaripotiwa kuja baada ya wiki iliyopita ripoti ya kampuni binafsi ya Price Waterhouse Coopers kubainisha kuwa zaidi ya dola milioni 26 ambazo zilikuwa zimeytengwa kwa ajili ya kuwasaidia Wakenya waliokuwa wakiaha kwa njaa zilitumbukia mifukoni mwa watu.
Kwa upande wa Wizara ya Elimu sakatai hilo lilianza kuibuka mwishoni mwa mwaka jana na hadi sasa kumekuwepo na ongezeko la shinikizo la kuwataka maofisa hao kujiuzulu.
Hata hivyo inaelezwa kuwa pamoja na kashifa hizo mbili hakuna Waziri wa Serikali hata mmoja ambaye amekwishapoteza kazi jambo ambalo linadaiwa kuwa ni ishara ya kuwa wanasiasa wengi Kenya hawapendi kuwajibika.
Inaelezwa kuwa hii siyo mara ya kwanza katika nchi hiyo iliyokithiri kwa rushwa kuona mtumishi wa Serikali akifuja mali ya umma lakini wanasiasa wakaendelea kubaki maofisini.(TAIFA LEO)
No comments:
Post a Comment