JOTI AKIWA KAZINI
Imedaiwa kuwa msanii huyo alikumbwa na mkasa huo baada ya kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kurekodi kipindi chao ambapo walemavu hao walipomkuta walianza kumfukuza na magongo yao wakitaka kumpiga nayo.
Kutokana na tafrani hiyo Joti alilazimika kuanza kutimua mbio huku na kule kwa nia ya kujiokoa maisha yake ambapo kwa bahati mbaya kulitokea gari iliyomganga na kumsababishia majeraha mwilini mwake.
Imedaiwa kuwa, walemavu hao walikuwa wamepanga kufanya mkutano katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo na baada ya kuzuia kufanya mkutano huo ndipo walipotawanyika na kila mmoja kwenda kijiweni kwake.
Walemavu hao katika madai yao makubwa ni kukanusha uvumi ambao unadaiwa kuwa mwanamke mmoja aliota manyoya mkononi kisha kutoweka kusikojulikana baada ya kumpa msaada katika tukio linalodaiwa kufanyika Salander Bridge.
Wakizungumza na PR HABARI baada ya maandamano yao mafupi walemavu hao kwa nyakati tofauti wamedai kuwa, tangu kuzuka kwa uvumi huo wamekuwa wakikumbana na vikwazo vingi sehemu wanazoishi na kwenye shughuli zao za kila siku.
Wamesema kuwa hivi sasa wamekuwa wakifuzwa kwenye nyumba walizopanga kwa madai kuwa, wanaotesha manyoya watu jambo ambalo si la kweli na linatakiwa kufutwa miongoni mwa jamii.
Mlemavu mmoja ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini amedai kuwa, hadi hivi sasa wenzao wawili wamefukuzwa katika nyumba walizokuwa wakiishi kwa madai kuwa ni washirikina.
Amedai kuwa, hata kipato chao cha siku kimeyumba kutokana na jamii kushindwa kuwasaidia kwa lolote kwa madai kuwa ni washirikina na wanaweza kuwaotesha manyoa.
" Tunaomba jamii ielewe kuwa hizo habari za mtu kuota manyoya si za kweli na tunaomba watu waendelee kutusaidia kwani sisi hatuna uwezo wa kutafuta fedha na tunahitaji msaada kutoka kwa watu mbalimbali,"alisema mlemavu huyo ambaye ana upofu wa macho.
Hivi karibuni kulizuka uvumi kuwa kuna mwanamke alikuwa akiendesha gari na baada ya kufika maeneo ya Sulander alimpa msaada ombaomba ambaye alimfuata kuomba msaada na baada ya kumpa aliota manyoa.
Taarifa hizo zilizagaa kwa kasi jijini na maeneo ya jirani ambapo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa ni za uzushi.
Inadaiwa kuwa baadhi ya watu walitumia uvumi huo kueneza ili jamii ishindwe kuwasaidia ombaomba hao kwa kuogopa kuota manyoa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Sebastian Masinde amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 5 asubuhi, Salandar Bridge wakati Joti na kundi la wasanii wenzake wakirekodi kipindi cha mwanamke kuota manyoya.
Amesema wakati wakiendelea na tukio hilo ndipo walipojitokeza walemavu ambao walihisi kuharibiwa soko na kuanza kuwatimua wasanii hao hali iliyosababisha lori lenye namba T 17 CD 118 mali ya ubalozi kumgonga Joti na kumsababishia majeraha mwilini mwake.
Uvumi wa mwanamke kuota manyoa
*Msanii wa Komedi Joti naye aonja joto ya jiwe
*Alazwa Muhimbili
MSANII maarufu wa Kikundi cha vichekesho la Orijino Komedi, Lucas Mhavile 'Joti' jana alikumbwa na kizaazaa baada ya kutinga katika eneo la Salandar akiwa na wasanii wenzake kwa ajili ya kurekodi kipindi cha uvumi ambapo inadaiwa kuwa, mwanamke mmoja aliota manyoya baada ya kutoa msaada kwa mlemavu mmoja aliyekuwepo maeneo hayo.
Imedaiwa kuwa msanii huyo alikumbwa na mkasa huo baada ya kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kurekodi kipindi chao ambapo walemavu hao walipomkuta walianza kumfukuza na magongo yao wakitaka kumpiga nayo.
Kutokana na tafrani hiyo Joti alilazimika kuanza kutimua mbio huku na kule kwa nia ya kujiokoa maisha yake ambapo kwa bahati mbaya kulitokea gari iliyomganga na kumsababishia majeraha mwilini mwake.
Imedaiwa kuwa, walemavu hao walikuwa wamepanga kufanya mkutano katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo na baada ya kuzuia kufanya mkutano huo ndipo walipotawanyika na kila mmoja kwenda kijiweni kwake.
Walemavu hao katika madai yao makubwa ni kukanusha uvumi ambao unadaiwa kuwa mwanamke mmoja aliota manyoya mkononi kisha kutoweka kusikojulikana baada ya kumpa msaada katika tukio linalodaiwa kufanyika Salander Bridge.
Wakizungumza na PR HABARI baada ya maandamano yao mafupi walemavu hao kwa nyakati tofauti wamedai kuwa, tangu kuzuka kwa uvumi huo wamekuwa wakikumbana na vikwazo vingi sehemu wanazoishi na kwenye shughuli zao za kila siku.
Wamesema kuwa hivi sasa wamekuwa wakifuzwa kwenye nyumba walizopanga kwa madai kuwa, wanaotesha manyoya watu jambo ambalo si la kweli na linatakiwa kufutwa miongoni mwa jamii.
Mlemavu mmoja ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini amedai kuwa, hadi hivi sasa wenzao wawili wamefukuzwa katika nyumba walizokuwa wakiishi kwa madai kuwa ni washirikina.
Amedai kuwa, hata kipato chao cha siku kimeyumba kutokana na jamii kushindwa kuwasaidia kwa lolote kwa madai kuwa ni washirikina na wanaweza kuwaotesha manyoa.
" Tunaomba jamii ielewe kuwa hizo habari za mtu kuota manyoya si za kweli na tunaomba watu waendelee kutusaidia kwani sisi hatuna uwezo wa kutafuta fedha na tunahitaji msaada kutoka kwa watu mbalimbali,"alisema mlemavu huyo ambaye ana upofu wa macho.
Hivi karibuni kulizuka uvumi kuwa kuna mwanamke alikuwa akiendesha gari na baada ya kufika maeneo ya Sulander alimpa msaada ombaomba ambaye alimfuata kuomba msaada na baada ya kumpa aliota manyoa.
Taarifa hizo zilizagaa kwa kasi jijini na maeneo ya jirani ambapo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa ni za uzushi.
Inadaiwa kuwa baadhi ya watu walitumia uvumi huo kueneza ili jamii ishindwe kuwasaidia ombaomba hao kwa kuogopa kuota manyoa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Sebastian Masinde amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 5 asubuhi, Salandar Bridge wakati Joti na kundi la wasanii wenzake wakirekodi kipindi cha mwanamke kuota manyoya.
Amesema wakati wakiendelea na tukio hilo ndipo walipojitokeza walemavu ambao walihisi kuharibiwa soko na kuanza kuwatimua wasanii hao hali iliyosababisha lori lenye namba T 17 CD 118 mali ya ubalozi kumgonga Joti na kumsababishia majeraha mwilini mwake.
No comments:
Post a Comment