header

nmb

nmb

Tuesday, February 23, 2010

WAIBUKA NA KUNENA......

rihanna


MWIMBAJI wa R&B nchini Marekani Rihanna ameibuka na kusema kuwa kukaa kwake kimya mbele za watu hakutokani na kuwaogopa.

Ilielezwa kuwa mwanadada huyo hajiambini hasa anapokutana na watu wageni kwake nandio maana hukaa kimya kwa muda mrefu.

Alijibu kwa kebehi akisema kuwa " sidhani kama fikra hizo zinaweza kuniatwala" na kuongeza kuwa hapendi kufungua mdomo wake mbele ya kila mtu.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na kituo cha redio cha WPGC na kuongeza kuwa watu wengi wanadhani kuwa anahofu, "huwa napenda kuchunguza, kutokana na hivyo wanadhani siwezi kuongea, sio kweli" alisema.



Aishwarya
MWANAMUZIKI wa kike nchini India Aishwarya Rai ameibuka na kupinga madai ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa alipata hofu na kutoendelea na matayarisho ya filamu yake mpya (jina kapuni) kutokana na hofu ya mauzo.

Alituma taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa sababu kubwa iliyomwondoa studio kwa sasa ni kutokana na maumivu makali ya tumbo na si vinginevyo.


Aishwarya alisema “sina hofu, napingana na taarifa iliyoandikwa gazetini, ni ya uzushi kabisa na kwa kweli imenikatisha tamaa," pia alilalamikia studio aliyokuwa akifanya nayo kazi kwa kitendo cha kutotoa maelezo yoyote kutokana na uzushi huo.
Hata hivyo, mkwe wake Amitabh Bahchcan alilalamikia kitendo cha baadhi ya vyombo vya habari kuandika taarifa zisizo na uthibitisho wowote.



No comments:

Post a Comment