MATESO UNDAVA WA FFU
BAADHI ya abiria wanaotumia kituo cha mabasi cha Ukonga, Mombasa, wamekilalamikia Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kitendo cha kuzifukuza daladala zilizokuwa zikitumia kituo cha hicho.
Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya abiria wamedai kuwa jana baadhi ya askari walikuwa wakiwafukuza madereva ili wasiegeshe magari katika kituo hicho na kusababisha vurugu.
Wamedai kuwa kutokana na hali hiyo abiria walilazimika kutembea mwendo mrefu kutoka Mombasa hadi kwa Diwani na Kivule.
“Hatufahamu kwanini FFU wamezuia daladala hizo kuegeshwa eneo hilo, jambo lililosababisha kero ya usafiri na kutembea mwendo mrefu,” alidai mkazi mmoja wa eneo hilo, Yahya Salumu.
Alidai kuwa kuna taarifa kuwa eneo la FFU linamalizikia kwenye uzio hivyo madereva wamekuwa wakilitumia eneo hilo kwa kupakiza abiria na kushusha na si kwa biashara.
“Tunaomba daladala ziendelee kupaki katika eneo hili kwani sisi wakazi wa Kivule na kwa Diwani zimekuwa zikitusaidia kuepukana na kero ya kutembea mwendo mrefu,” amedai mkazi wa Mazizi Ukonga Asha Mfaume.
Amedai kuwa kutokana na hali hiyo hivi sasa baadhi ya wakazi wanalazimika kutembea kwa miguu hivyo wameuomba uongozi wa Kata ya Ukonga kuingilia katia suala hili.
Wamedai kuwa kama kuna uwezekano ni bora madereva hao wakaelezwa sehemu ya kuegesha magari yao ili kuendelea na biashara hiyo.

No comments:
Post a Comment