header

nmb

nmb

Wednesday, January 11, 2012

MZEE KIPALA AFARIKI DUNIA !!Msanii Mkongwe katika tasnia ya Maigizo/Filamu hapa nchini, Fundi Saidi almaarufu kwa jina la kisanii Mzee Kipara amefariki mapema leo asubuhi,nyumbani kwake huko Kigogo Mbuyuni-Kinondoni jijini dar.

Mzee kipara ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1922,huko Bongoni mkoani Tabora,alikuwa kisumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu,alikuwa hawezi kusimama mwenyewe,sambamba na umri nao huenda ulichangia kwa maradhi hayo na mengineyo,hali iliyokuwa ikimlazimu kutumia muda mwingi kitandani,wakati mwingine alishindwa kutoka nje mpaka watu watokee kumtoa nje ili kuota jua ama kupunga upepo.

No comments:

Post a Comment