header

nmb

nmb

Wednesday, January 18, 2012

KIKAO CHA KUMJADILI MZEE KIHAKA ANAYETUHUMIWA KUBAKA MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 12 WAKAZI HAO WATAKA MZEE HUYO ASIKANYAGE TENA KWENYE KATA!!

 1. Kikongwe huyu Asangwile Kihaka miaka 78 ndiye anayetuhumiwa kubaka mwanafunzi wa miaka 12 anayesoma shule ya msingi mbata jijini Mbeya


  Huyu ni mzazi wa binti aliyebakwa na mzee Asangwile Kihaka mzazi huyu wa binti aligoma kabisa kusogea kwenye mkutano huo cha wakazi wa Ghana...


  Diwani wa Kata Ghana Bwana Anjelo Chavaligino akijitetea kwa wakazi wake sabababu ya kutofika katika kikao cha kwanza cha kumjadili mzee Kihaka...


  Mtendaji wa kata ya Ghana akishindwa kujibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na wananchi kuwa kwanini alitoa barua ya kwenda kumwekea mdhamana anayedaiwa kubaka mtoto...  Mtendaji wa kata hiyo akiwa amekasirika alikataa hata kufunga kikao ambacho nacho kilivurugika...


  Moja wa asakari aliyekuwa akilinda usalama wa kikao hicho akishangiliwa na wakazi wa Ghana na mbata kwa kusema sheria ipo na itachukua mkondo wake na mzee Kihaka hatarudi tena kwenye mji wake...


  Wazee kwa vijana na watoto wote walikusanyika katika ofisi mtendaji kata ya Ghana kusikiliza taarifa ya anayetuhumiwa kubaka...


  Wakazi wa Mbata na Ghana wakiwa makini kumsikiliza mh diwani wao...


  Huku kikao cha kumjadili mzee Kihaka kikiendelea naye dada huyu alikuwa pembeni akiwakanya na kuwafundisha jinsi gani ya kuwaepuka wabakaji na kuacha tabia ya kuombaomba hela kwani ndiyo inayowapelekea wabakaji kuwatamani...


  Watoto nao hawakukosa katika kikao hicho cha kumjadili mzee Kihaka anayetuhumiwa kubaka binti wa miaka 12


  Hii ndiyo nyumba ya mzee Asangwile Kihaka ambayo wakazi wa Ghana waliishambulia kwa mawe na kuvunja vioo vya nyumba hiyo. Imetoka Mbeyayetublog.kwa hisani ya blog ya kif:

No comments:

Post a Comment