header

nmb

nmb

Saturday, April 10, 2010

MATUKIO YA VIFO MWANZO MWA WIKIENDI

MTOTO KAMA HUYU HAPASWI KUTUPWA ANAHITAJI UPENDO KWANI KUNA VITUO VYA KUWATUNZA KAMA HUWEZI KUWATUNZA USIWATUPE TULETEE HAPA


MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule ya msingi kunduchi amekufa baada ya kutumbukia katika mto wakati akiwa anavuka.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Bw. Elias Kalinga alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 12 jioni tegeta msichoke.
Kamanda alimtaja mtoto huyo kuwa ni Victor Madiga (10) na inadawia kuwa alitumbukia katika mto huo wakati akijaribu kuvuka.

Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.

Katika tukio lingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Bw. Faustine Shilogile alisema kuwa mtoto Josha Stepheno (4) amekufa baada ya kutubukia katika dimbwi la maji ya mvua.

Alisema tukio hilo lilitokea saa 8 mchana katika maeneo ya majowe shule ya msingi mjimpya na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Amana.

WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti yaliyotokea jijini Dar es Salaam likiwemo la mtoto mchanga aliyeuawa na mtu asiyefahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile amesema kuwa, tukio la kwanza limetokea jana saa 12 jioni, Vingunguti Bonde la Msimbazi.

Amesema kuwa, maiti ya mtoto huyo wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja pia imeweka katika hospitari ya Amana


Inatisha sana mazee.Imeletwa na Msomaji wetu

No comments:

Post a Comment