header

nmb

nmb

Tuesday, March 12, 2013

JK AMJULIA HALI MZEE YUSUFU MZIMBA WA YANGA

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee maarufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na bodaboda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi juzi hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka.
(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment