MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinachoonyesha kuwa petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.
“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa hiyo.
Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya taa Sh1,973.
Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa Sh2,057.
Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122.
Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita.
“Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia 6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema.
Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko. “Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,” alisema Masebu.
Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo kikomo.
Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema.
Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

EWURA yatangaza Bei Kikomo za Mafuta aina ya Petroli nchini
KUMB: PPR/13 - 1/1
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA
JUMATANO, TAREHE 2 JANUARI 2013
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),
inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 2 Januari 2013. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo. |
(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 05 Desemba 2012. Katika toleo hili, bei za rejareja kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 126/lita sawa na asilimia 5.96; Dizeli Sh 32/lita sawa na asilimia 1.60; na Mafuta ya Taa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.50. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 126.10/lita sawa na asilimia 6.17; Dizeli kwa Sh 32.48/lita sawa na asilimia 1.69; na Mafuta ya Taa kwa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.6. Mabadiliko haya ya bei yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.
(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
(e) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.
A: BEI ZA REJAREJA
Bei Kikomo
| |||
Mji
|
Petroli
|
Dizeli
|
Mafuta ya Taa
|
(Tsh/Lt)
|
(Tsh/Lt)
|
(Tsh/Lt)
| |
Dar es Salaam
|
1,993
|
1,967
|
1,973
|
Arusha
|
2,077
|
2,051
|
2,057
|
Arumeru (Usa West)
|
2,077
|
2,051
|
2,057
|
Karatu
|
2,095
|
2,069
|
2,075
|
Monduli
|
2,082
|
2,056
|
2,062
|
Ngorongoro (Loliondo)
|
2,133
|
2,107
|
2,113
|
Kibaha
|
1,997
|
1,972
|
1,977
|
Bagamoyo
|
2,004
|
1,978
|
1,984
|
Kisarawe
|
2,000
|
1,974
|
1,980
|
Mkuranga
|
2,002
|
1,977
|
1,982
|
Rufiji
|
2,020
|
1,995
|
2,000
|
Dodoma
|
2,051
|
2,026
|
2,031
|
Bahi
|
2,059
|
2,033
|
2,039
|
Chemba
|
2,078
|
2,052
|
2,058
|
Kondoa
|
2,084
|
2,058
|
2,064
|
Kongwa
|
2,049
|
2,023
|
2,029
|
Mpwapwa
|
2,052
|
2,027
|
2,032
|
Iringa
|
2,057
|
2,031
|
2,037
|
Kilolo
|
2,061
|
2,035
|
2,041
|
Mufindi (Mafinga)
|
2,067
|
2,041
|
2,047
|
Njombe
|
2,085
|
2,059
|
2,065
|
Ludewa
|
2,123
|
2,097
|
2,103
|
Makete
|
2,116
|
2,090
|
2,096
|
Wanging'ombe (Igwachanya)
|
2,083
|
2,057
|
2,063
|
Bukoba
|
2,208
|
2,182
|
2,188
|
Biharamulo
|
2,182
|
2,156
|
2,162
|
Karagwe (Kayanga)
|
2,224
|
2,198
|
2,204
|
Kyerwa (Ruberwa)
|
2,230
|
2,204
|
2,210
|
Muleba
|
2,208
|
2,182
|
2,188
|
Ngara
|
2,173
|
2,147
|
2,153
|
Misenyi
|
2,216
|
2,190
|
2,196
|
Geita
|
2,158
|
2,132
|
2,138
|
Bukombe
|
2,147
|
2,121
|
2,127
|
Chato
|
2,179
|
2,153
|
2,159
|
Mbogwe
|
2,196
|
2,170
|
2,176
|
Nyang'hwale
|
2,173
|
2,147
|
2,153
|
Kigoma
|
2,223
|
2,198
|
2,203
|
Uvinza (Lugufu)
|
2,236
|
2,210
|
2,216
|
Buhigwe
|
2,213
|
2,187
|
2,193
|
Kakonko
|
2,181
|
2,155
|
2,161
|
Kasulu
|
2,210
|
2,184
|
2,190
|
Kibondo
|
2,188
|
2,162
|
2,168
|
Moshi
|
2,066
|
2,041
|
2,046
|
Hai (Bomang'ombe)
|
2,069
|
2,044
|
2,049
|
Mwanga
|
2,059
|
2,034
|
2,039
|
Rombo (Mkuu)
|
2,087
|
2,061
|
2,067
|
Same
|
2,053
|
2,027
|
2,033
|
Siha (Sanya Juu)
|
2,073
|
2,047
|
2,053
|
Lindi
|
2,051
|
2,026
|
2,031
|
Kilwa Masoko
|
2,026
|
2,001
|
2,006
|
Liwale
|
2,072
|
2,047
|
2,052
|
Nachingwea
|
2,081
|
2,055
|
2,061
|
Ruangwa
|
2,079
|
2,053
|
2,059
|
Babati
|
2,115
|
2,089
|
2,095
|
Hanang (Katesh)
|
2,125
|
2,100
|
2,105
|
Kiteto (Kibaya)
|
2,126
|
2,100
|
2,106
|
Mbulu
|
2,127
|
2,102
|
2,107
|
Simanjiro (Orkasumet)
|
2,147
|
2,121
|
2,127
|
Musoma
|
2,171
|
2,145
|
2,151
|
Rorya (Ingirijuu)
|
2,180
|
2,154
|
2,160
|
Bunda
|
2,162
|
2,136
|
2,142
|
Butiama
|
2,168
|
2,142
|
2,148
|
Serengeti (Mugumu)
|
2,216
|
2,191
|
2,196
|
Tarime
|
2,182
|
2,156
|
2,162
|
Mbeya
|
2,099
|
2,074
|
2,079
|
Chunya
|
2,109
|
2,083
|
2,089
|
Ileje
|
2,113
|
2,087
|
2,093
|
Kyela
|
2,115
|
2,090
|
2,095
|
Mbarali (Rujewa)
|
2,084
|
2,058
|
2,064
|
Mbozi (Vwawa)
|
2,109
|
2,083
|
2,089
|
Momba (Chitete)
|
2,118
|
2,092
|
2,098
|
Rungwe (Tukuyu)
|
2,108
|
2,083
|
2,088
|
Morogoro
|
2,018
|
1,992
|
1,998
|
Mikumi
|
2,033
|
2,008
|
2,013
|
Kilombero (Ifakara)
|
2,055
|
2,030
|
2,035
|
Ulanga (Mahenge)
|
2,066
|
2,040
|
2,046
|
Kilosa
|
2,036
|
2,010
|
2,016
|
Mvomero (Wami Sokoine)
|
2,028
|
2,002
|
2,008
|
Mtwara
|
2,065
|
2,039
|
2,045
|
Nanyumbu (Mangaka)
|
2,114
|
2,088
|
2,094
|
Masasi
|
2,090
|
2,065
|
2,071
|
Newala
|
2,097
|
2,071
|
2,077
|
Tandahimba
|
2,090
|
2,064
|
2,070
|
Mwanza
|
2,142
|
2,117
|
2,122
|
Kwimba
|
2,178
|
2,153
|
2,158
|
Magu
|
2,150
|
2,125
|
2,130
|
Misungwi
|
2,148
|
2,122
|
2,128
|
Sengerema
|
2,175
|
2,149
|
2,155
|
Ukerewe
|
2,202
|
2,176
|
2,182
|
Sumbawanga
|
2,165
|
2,139
|
2,145
|
Kalambo (Matai)
|
2,158
|
2,132
|
2,138
|
Nkasi (Namanyele)
|
2,179
|
2,153
|
2,159
|
Katavi (Mpanda)
|
2,200
|
2,174
|
2,180
|
Mlele (Inyonga)
|
2,178
|
2,153
|
2,158
|
Songea
|
2,116
|
2,090
|
2,096
|
Mbinga
|
2,149
|
2,124
|
2,129
|
Namtumbo
|
2,145
|
2,119
|
2,125
|
Nyasa (Mbamba Bay)
|
2,152
|
2,126
|
2,132
|
Tunduru
|
2,175
|
2,149
|
2,155
|
Shinyanga
|
2,121
|
2,096
|
2,101
|
Kahama
|
2,135
|
2,109
|
2,115
|
Kishapu
|
2,150
|
2,124
|
2,130
|
Simiyu (Bariadi)
|
2,163
|
2,137
|
2,143
|
Busega (Nyashimo)
|
2,156
|
2,130
|
2,136
|
Itilima (Lagangabilili)
|
2,166
|
2,140
|
2,146
|
Maswa
|
2,154
|
2,128
|
2,134
|
Meatu (Mwanhuzi)
|
2,161
|
2,135
|
2,141
|
Singida
|
2,083
|
2,057
|
2,063
|
Iramba
|
2,095
|
2,070
|
2,075
|
Manyoni
|
2,068
|
2,042
|
2,048
|
Ikungi
|
2,079
|
2,053
|
2,059
|
Mkalama (Nduguti)
|
2,108
|
2,082
|
2,088
|
Tabora
|
2,147
|
2,121
|
2,127
|
Igunga
|
2,101
|
2,075
|
2,081
|
Kaliua
|
2,165
|
2,139
|
2,145
|
Ulyankulu
|
2,159
|
2,133
|
2,139
|
Nzega
|
2,111
|
2,085
|
2,091
|
Sikonge
|
2,158
|
2,133
|
2,138
|
Urambo
|
2,160
|
2,134
|
2,140
|
Tanga
|
2,039
|
2,013
|
2,019
|
Handeni
|
2,018
|
1,992
|
1,998
|
Kilindi
|
2,053
|
2,027
|
2,033
|
Korogwe
|
2,032
|
2,006
|
2,012
|
Lushoto
|
2,041
|
2,016
|
2,021
|
Mkinga (Maramba)
|
2,053
|
2,027
|
2,033
|
Muheza
|
2,039
|
2,013
|
2,019
|
Pangani
|
2,045
|
2,020
|
2,025
|
B: BEI ZA JUMLA
Bei za Jumla - DSM
|
Petroli (Sh/L)
|
Dizeli (Sh/L)
|
Mafuta ya Taa (Sh/L)
|
Bei Kikomo
|
1,918.60
|
1,892.97
|
1,898.62
|
Haruna Masebu
MKURUGENZI MKUU
No comments:
Post a Comment