header

nmb

nmb

Thursday, April 21, 2016

BONDIA WA KIKE LULU KAYAGE AHAPA KUFIA URINGONI KATIKA MPAMBANO WAKE MEI 14 TAIFA


BONDIA CHIEDZA HOMAKOMA 'NIKITA' MALAWI  LULU KAYAGE TANZANIA

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Lulu Kayage yupo katika mazoezi mazito na makali kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake wa kimataifa na Chiedza Homakoma 'Nikita' Malawi mpambano utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa 

akizungumza wakati wa mazoezi yake anayofanya kinondoni msisiri amesema anajiandaa vizuri tu kwa ajili ya kumkabili mmalawi huyo atakaepigana nae 

aliongeza kwa kusema unajuarekodi yangu imearibika kidogo kwa kuwa nilipigwa kwa point mpambano wangu wa mwisho

hivyo sasa nimejipanga vizuri kuakikisha nafanya vema katika mpambano uho wa kimataifa nawa aidi mashabiki wagu kuwa siku hiyo nitakuwa radhi nifie uringoni ili ushindi ubaki Tanzania na siwezi kupigwa hapa nchini na nikatia aibu Taifa langu

siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi nchini

ambapobondia Thomas Mashali atakumbana na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani'  ubingwa wa Dunia mkanda wa U.B.O 

mapambano mengine ya kimataifa yatawakuanisha bondia Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi  wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya  na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda

mapambano mengini ni kati ya Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola

mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga




siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo

No comments:

Post a Comment