header

nmb

nmb

Friday, March 4, 2016

Wateja wa Fastjet kununua tiketi za usafiri kupitia Airtel Money


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kulia), akipongezana na Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse baada ya Airtel na Fastjet kuingia ubia wa kibiashara utakaowawezesha  Wateja wa Fastjet kununua tiketi za usafiri kupitia Airtel Money, katika  hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana katika ofisi za Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kununua tiketi za ndege za Fastjet kupitia Airtel Money. (kushoto) Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse (kulia) ni Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa.
Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse (kushoto)  akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Fastjet na Airtel utakaowawezesha  Wateja wa Fastjet kununua tiketi za usafiri kupitia Airtel Money. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na  Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya  akimpongeza mmoja wa waandishi wa habari wa clouds TV  James Lyatuu mara baada ya kuibuka mshindi wa tiketi ya bure ya fastjet  wakati wa uzinduzi wa ubia wa kampuni ya Airtel na Fastjet utakaowawezesha wateja kulipia tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya  akimpongeza  Mpigapicha za habari wa The Guardian Ltd na Media Solutions , John Badi  baada ya kuibuka mshindi wa tiketi ya bure ya fastjet  wakati wa uzinduzi wa ubia wa kampuni ya Airtel na Fastjet utakaowawezesha wateja kulipia tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money
 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
 · Lipa tiketi ya Fastjet kwa Airtel Money upate tiketi ya bure
Dar es Salaam Machi 01, 2016- Kampuni ya ndege ya ki-Afrika yenye gharama nafuu Fastjet, imekuwa ya kwanza kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania ambapo wateja wa Fastjet wataanza kununua tiketi na hata kufanya miamala mingine kupitia Airtel Money.
Kutokana na makubaliano hayo, wateja wa fastjet watakaoununua tiketi kupitia Airtel Money, watapata nafasi ya kushinda tiketi ya kusafiri wa ndani na nje ya nchi kupitia droo ambayo itafanywa kwa miezi miwili.
Akitangaza kusainiwa kwa makubaliano hayo, Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse alisema: “ukweli kwamba wateja wetu watamudu kupata tiketi zao kupitia Airtel Money kunaimarisha kujituma kwetu katika  kuhakikisha kuwa Fastjet inaishi kulingana na ahadi yake ya kuwa shirika lisilo na usumbufu linalofanya safari za wateja wake kuwa ni rahisi.
Alisema kuwa huduma hiyo ambayo inampa mteja uhakika wa kupata tiketi za Fastjet kutoka mahali alipo kwa kutumia  simu za mkononi, itaanza Machi 03, 2016 na kuongeza kuwa mpango huo mpya wa kushirikiana na Airtel  sio tu kwamba utahakikisha kuwa huduma inakuwa ya kasi na ya ufanisi bali pia itaondoa kabisa kadhia ya kupoteza muda miongoni mwa wateja walipokuwa wanakwenda kununua tiketi kutoka kwa mawakala wa Fastjet waliopo mbali na makazi yao.
“Tunajivunia mno na tunawashukuru wateja wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono na tunaahidi kuendelea kuwapa huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu pamoja na kusikiliza mahitaji ya wateja wetu,” alisema Corse.
Akizungumza kuhusu makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya alisema: “ushirikiano huu umekuwa ni njia sahihi kwa wateja wetu ya kulipia tiketi kwa safari zao za ndani na za kimataifa wakati wowote, mahali popote kwa utulivu wakiwa majumbani kwa kutumia  simu ya mkononi.
 “Tunaamini wateja wetu wa Airtel Money  kote nchini  hivi sasa watafurahia  njia hii ya haraka na rahisi kulipia  na hali kadhalika  kupanga safari zao na Fastjet katika mazingira ya utulivu.”
Aliongeza kusema, “Airtel itaendelea kuonesha  kujituma kwake katika kutoa bidhaa na huduma zilizojikita kwenye ubunifu, kuanzisha ushirikiano ambao ni muhimu na utakaokidhi mahitaji ya wateja kupitia huduma za Airtel Money  wakati wowote.”
Akiongelea promosheni hiyo, Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa alisema, “tutakuwa tunatoa zawadi kwa wateja watakaonunua tiketi za fastjet kupitia Airtel Money kila baada ya wiki mbili kwa miezi miwili. Tiketi hizi zitatolewa kupitia droo ambapo kumi na sita zitakuwa za safari za ndani ya nchi na nne zitakuwa za safari za nje ya nchi. Tunawaomba wateja kununua tiketi kupitia Airtel Money ili wapate nafasi ya kushinda tiketi za safari wazipendazo”, alisema Nalingiwa.
Nalingiwa alibainisha: “Ili kulipia tiketi, mteja anatakiwa kupiga: *150*60*#, halafu chagua, ‘lipia bili’, halafu, ‘chagua kwenye orodha’, halafu chagua, ‘Usafiri wa anga’, kisha ufuate maagizo”.
Kuhusu Bharti Airtel
Bharti Airtel Limited ni kampuni ya mawasiliano ya simu  inayoongoza duniani  ikiwa inafanya shughuli zake   miongoni mwa nchi 20 barani Asia na Afrika. Makao yake makuu ni New Delhi, India, ikiwa ni kampuni inayoshika nafasi ya tatu miongoni mwa makapauni yanayotoa huduma ya simu duniani. Nchini India, kampuni inatoa bidhaa mbalimbali  zikiwemo huduma za intaneti bila nyaya za 2G, 3G na 4G, biashara kwa njia ya simu, huduma za njia ya simu, huduma ya kasi ya DSL broadband, IPTV, DTH, huduma za ujasiriamali  zikiwemo huduma  ya usafirishaji masafa marefu kitaifa na kimataifa. Kwenye maeneo mengine ya kijiografia  inatoa huduma za intaneti bila nyaya na biashara kwa njia ya simu. Bharti Airtel ilikuwa na wateja zaidi ya milioni 335 kwenye maeneo inakoendesha shughuli zake hadi kufikia mwishoni mwa Agosti 2015. Ili kufahamu zaidi tembelea wavuti wake, www.airtel.com
Kuhusu Fastjet Tanzania
Fastjet Tanzania ni kampuni ya ndege yenye gharama nafuu iliyoanza safari zake nchi Tanznaia November 2012. Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya usalama, ubora, ulinzi na uhakika , Fastjet imeleta uzoefu mpya wa kusafiri kwenye soko la Afrika katika kiwango cha bei ya chini. Kwa kutumia ndege zake za Airbus A319 Fastjet  imekuwa inatumia bei ya chini Afrika na mikakati yake ya muda mrefu ni kuwa kampuni ya kwanza ya ndege Afrika ya gharama nafuu.
Matokeo ya utafiti kuhusu kuridhika kwa wateja yanaonesha kuwa asilimia 100 ya wateja wanaweza kusema kuwa wanapendezeshwa na huduma za Fastjet. Katika kuendeleza nembo na utambulisho wake, Fastjet imeshateuliwa kwa ajili ya tuzo kadhaa, ukiwemo ushindi wa tuzo tatu za ‘kujisuka upya ki-biashara’ (re-branding) na uzinduzi wa Fastjet ambayo unafahamika kama "Brand Strategy of the Year"  uliyopatikana kwenye Tuzo za Masoko za Drum jijini London na Tuzo ya Mbunifu wa Usafiri  kwenye Tuzo za Nane za Usafiri Afrika 2015 Johannesburg.   

No comments:

Post a Comment