header

nmb

nmb

Friday, February 26, 2016

MAZISHI YA MZEE MAPILI KUFANYIKA KISUTU LEO!


Kwa mujibu wa Mkwe wa marehemu, Wema Mustapha Mgombelwa 'Baba Wawili" shughuli za mazishi ya marehemu Mzee Mapili zitafanyika Magomeni Mapipa Mtaa wa Magomeni Namba 21. 

Wema alisema: "Tunaweza kumzika katika makaburi ya Mwinyimkuu au Kisutu jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa),."
Mkwe huyo ambaye ni seneta maarufu wa Bendi ya Msondo Ngoma alisema mkwe wake alifariki Jumanne usiku baada ya kutoka kuangalia mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Arsenal na Barcelona.
"Kikubwa alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu, alifariki usiku na maiti yake imepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Baada ya kupata taarifa za msiba huo tunawaomba ndugu jamaa na marafiki kujumuika pamoja katika mazishi ya kumhifadhi mzee wetu," alisema Wema.

No comments:

Post a Comment