header

nmb

nmb

Thursday, January 24, 2013

BREAKING NEWS: TAARIFA ZA USIKU HUU KUTOKA MSIMBATI MTWARA GARI LILILOTAKA KUMTOROSHA KIKONGWE ALIYETOA AHADI GESI IKISAFIRISHWA MABOMBA YATATOA MAJI LACHOMWA MOTO.

Bibi Somoe Issa kushoto, kulia ni mwanidhsi wa habari wa info radio mjini Mtwara.
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kua Gari lililotaka Kumtorosha Bibi wa Kijiji cha Msimbati Bi Somoe Issa, alietoa ahadi kuwa gesi ikisafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam itageuka Maji limechomwa Moto Usiku huu huko Msimbati. Habari zinaeleza kuwa ulinzi mkali umeimarishwa nyumbani kwa bibi huyo. Taarifa zaidi tutawaletea asubuhi kadri tutakavyo zipata kutoka eneo la tukio. 
 Kikongwe Somoe Issa anayekadriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 90 ambaye ni Mkuu wa Kaya ya Msimbati kijiji ambacho gesi asilia inavunwa, mkoani Mtwara aliionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi

No comments:

Post a Comment