MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI PADRI AMBROSE MKENDA ALIYELAZWA MUHIMBILI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Padri Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi mwangalizi wa mgonjwa huyo,
KLABU ZA JOGGING JIJINI DAR ZAAGA MWAKA KWA BONANZA , MBUNGE WA KINONDONI ASHIRIKI AWAAMBIA HAKUNA SABABU YAKWENDA LOLIONDO MAZOEZI YANATOSHA.
Vijana wa Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni wakifanya mazoezi kwenye bonanza hilo. |
Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam ikivutwa na Timu ya Klabu ya Jogging ya Kawe na kuondolewa.
|
MTU MMOJA AJERUHIWA MADARASA SITA YAEZULIWA NA UPEPO.
Bati zilizoezuliwa na upope huo mkali ulioacha athari kubwa. |
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo. |
Waziri Mkuu Ahimiza Maendeleo Jimboni Katavi.
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anapata maelezo kutoka kwa mtalamu wa Tanesco makao makuu Eng. Tumaini Temu kuhusu jinsi jenereta walil lifunga linavyofanya kazi katika kuzalisha umeme katika kijiji cha Kibaoni.kushoto kwa waziri mkuu ni tekinisheni wa Tanesco Bibi.Salama Mpera.
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anakagua kibanda kilichojengwa kwa ajili ya kuweka jenereta la kufua umeme katika kijiij cha Kibaoni Katavi Mh.waziri mkuu yupo katika ziara ya kukukagua shughuli za maendeleo na mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya kijijini kwao Kibaoni Katavi.
Mh.Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika shamaba lake katika kijiji cha Kibaoni Katavi akiangalia mahindi yalivyostawi.
Bwana Godfrey Pinda ambaye ni mdogo wa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anamwelezea Waziri Mkuu kuhusu anavyolima kilimo cha mananasi minazi katika shamba lake katika kijiji cha Kibaoni Katavi Waziri mkuu yupo katika jimbo lake la Katavi katika kukagua shughuli za maendeleo pamoja na mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya.
(Picha na Chris Mfin
IBF YAMTANGAZA LUCAS RUTAINURWA WA KITWE GENERAL TRADERS KAMA PROMOTA WA MWAKA 2012
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati limemtamngaza bwana Lucas Rutainurwa wa kampuni ya Kitwe General Traders ya jijini Dar-Es-Salam kama Promota wa mwaka 2012.
Akitangaza habari hizi, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi alisema kuwa bwana Lucas Rutainurwa alifanikisha Watanzania wawili kuwa mabingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi an Mashariki ya Kati mwaka unaoishia Desemba 2012.
Katika harakati zake za kuipa Tanzania sura ya kimataifa katika tasnia ya ngumi za kulipwa Rutainurwa na kampuni yake ya Kitwe General Traders waliandaa mapambano makubwa mawili ambayo yalizidi maandalizi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika Tanzania kwa miaka ya karibuni.
Mwezi April mwaka 2012, Rutainurwa na Kitwe General Traders waliandaa pambano lililowakutanisha mabondia Francis Cheka na Mada Maugo wote wa Tanzania kugombea mkanda wa IBF bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika ukumbi wa PTA jijini Dar-Es-Salaam. Katika mpambano huo bondia Francis Cheka aliibuka kidedea baada ya kumsimamisha Maugo katika raundi ya nane.
Francis Cheka alitetea vyema mkanda wake huo tarehe 26 Desemba jijini Arusha alishinda kwwa points bondia Chimwemwe Chiotcha kutoka nchini Malawi katika pambano lao la raundi 12.
Mwezi wa nane mwaka 2012, Rutainurwa na Kitwe General Traders waliandaa mpambano mwingine kati ya bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania na Sunday Kizito kutoka Uganda kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito wa Unyoya (Featherweight).
Katika mpambano huo bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania alimsimamisha Sunday Kizito kutoka Uganda katika raundi ya 9 na kutangazwa kuwa bingwa mpya wa IBF.
Kupatikana kwa mabingwa hao, kumeifanya Tanzania kuwa nyumbani kwa mabingwa wawili wa IBF na hivyo kuiweka nchi hii katika ngazi moja na chache duniani hususa katika bara la Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini, Ghana, Morocco, Algeria na Cameron.
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa lina makao yake makuu yanayoratibu bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati kutokea katika jiji la Dar-Es-Salaam, Tanzania. Hii ni heshima ya kipekee kwa nchi ya Tanzania kwani nchi nyingi zinagombania kuwa makao makuu ya shirikisho hii kubwa kuliko yote duniani.
IBF imemshukuru sana bwana Lucas Rutainurwa na kampuni yake ya Kitwe General Traders kwa mafanikio haya mazuri.
Bwana Lucas atapewa tuzo yake la kuwa promota wa mwaka wa IBF katika bara la Afrika mwaka 2012 rasmi wakati wa mkutano wa 30 wa IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin, nchini Ujerumani Mai mwakani.
Katika hatua nyingine:
Bwama Michael Tetteh na bwana Henry Many-Spain wa GoldMike Promotions and Golden Concept za jiji la Accra, Ghana wameteuliwa kama promota wa mwaka 2012 wa mapambano ya IBF ya mabara. Bwana Tetteh amepromoti mapambano mengi ya IBF ya mabara (Continental Titles) kuliko promota mwingine yeyote katika bara la Afrika.
Aidha, IBF imemteua bwana Branco Milenkovik wa kampuni ya Branco Sports Productions ya jiji la Johannesburg, nchini Afrika ya Kusini kama promota wake wa mwaka wa mapambano ya dunia mwaka 2012. Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Branco kuteuliwa kama promota wa mwaka kwa kuandaa mapambano mengi ya IBF ya ubingwa wa dunia.
Imetolewa na:
Makao ma
Saturday, December 29, 2012
Arusha Kuwa Makao Makuu Ya Chama Cha Ngumi Za Kulipwa Afrika Ya Mashariki Na Kati (ECAPBA).
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 29/12/2012
Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimepata nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Gaudence Lyimo kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, EAC”
Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa ECAPBA itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Juhudi za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
Uamuzi huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama waECAPBA bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
Nchi ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika.
Imetumwa na:
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Makazi ya padri Ambrose Mkenda Paroko wa kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar na kuupa pole uongozi wa Kanisa hilo pamoja na Familia yake kufwatia ajali ya kupigwa risasi hivi karibuni na watu wasioujulikana na Pia Akagua gari ya Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda ambayo alikuwa akiendesha na kuvamiwa kwa risasi ya watu wasiojuilikana
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia gari ya Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda ambayo alikuwa akiendesha na kuvamiwa kwa risasi ya watu wasiojuilikana
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Uongozi wa Skuli ya Francis Maria Tomondo ambapo Padre Ambrose Mkenda wa Paroko ya Parokia ya Mpendae alijeruhiwa kwa risasi hivi karibuni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Father Shayo wa Kanisa la Roman Catholic liliopo minara miwili baada kuwafariji na kutoa mkono wa pole kwa uongozi wa huo kufuatia kujeruhiwa kwa Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda.
---
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika makazi ya padri Ambrose Mkenda wa Paroko wa parokia ya kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar kuupa pole uongozi wa Kanisa hilo pamoja na Familia yake kufuatia ajali ya kupigwa risasi hivi karibuni na watu wasioujulikana.
Tukio hilo la kusikitisha lililofanywa na watu wawili waliopakiana kwenye Vespa lilitokea langoni mwa Skuli ya Francis Maria iliyopo Tomondo Wilaya ya Magharibi ambapo ndio makaazi ya Padri Ambrose.
Balozi Seif akiufariji Uongozi huo alisema ni jambo baya na la kusikitisha lililofanywa na watu hao ambalo limetoa sura mbaya kwa Taifa na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo na haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria watu watakaobainika kufanya uhalifu huo.
Alisema Serikali imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika hali ya wasi wasi usio wa lazima ndani ya harakati zao za kimaisha.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi na Familia ya Padre Ambrose Mkenda Kiongozi kutoka Kanisa la Roman Catholic Father Shayo aliiomba Serikali kuendelea kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu iliyotanda mioyoni mwao kutokana na matukio ya uvamizi.
Father Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa sababu ya utofauti wa Kidini inawajengea maisha mabovu watoto hao. “ Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine tuelewe kwamba Taifa halitakuwa na muelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye”. Alitahadharisha Father Shayo.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment