TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUZINDULIWA KWA KINYWAJI CHA ZANZI CREAM LIQUEUR
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited wazalishaji wa bidhaa bora zaidi za vinywaji vikali na mvinyo hapa nchini, kwa mara nyingine tena inapenda kutambulisha bidhaa yake mpya ambayo ni kinywaji chenye radha nzuri kabisa kiitwacho Zanzi Cream Liqueur.
Kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kinazalishwa na Tanzania Distilleries Limited, hivyo kuwa kinywaji cha kwanza katika vinywaji vya jamii ya Cream Liqueur kuzalishwa nchini Tanzania na kampuni ya humu nchini na kuingia katika soko la kimataifa kama vilivyo vinywaji vingine vya aina hiyo vinavyozalishwa kutoka nje.
Zanzi Cream Liqueur ni kinywaji cha watu wa aina zote ingawa uzoefu unaonekana aina hiyo ya vinywaji vinapendwa zaidi na wanawake, kutokana na radha yake, humfanya mnywaji ajisikie mwenye furaha muda wote na mambo mengi ya kuvutia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa alisema, ana uhakika kinywaji hicho kitapendwa na wengi kwani ni cha Kitanzania, na kuwa TDL imezingatia ubora wa kiwango cha Kimataifa katika kuzalisha kinywaji cha Zanzi Cream liqueur.
Mgwassa aliwataka Watanzania kujivunia kinywaji hicho, ambacho kimezinduliwa leo na kusema TDL ikiwa ni kampuni ya kizalendo itaendelea kuhakikisha inazidi kuitangaza Tanzania kwa kuzalisha bidhaa bora zinazopendwa na wengi ndani na nje ya nchi.
“Kwetu sisi TDL tunajivunia kuzindua rasmi kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kwani kinazalishwa na Watanzania na kimebuniwa na wazalendo wa nchi hii, huu sasa ni wakati wa kutembea mbele kujivunia kinywaji hiki na naamini kitavutia wengi kutokana na jinsi kilivyotengenezwa na ubora usio na shaka.”
Mgwassa alisema, nia ya kuzalisha kinywaji cha Zanzi Cream Liquer ni baada ya kuona kuna vinywaji vingi vya aina hiyo vikiingizwa nchini kutoka nje hivyo, TDL ikataka kuzalisha bidhaa bora zaidi na ya kipekee hapa duniani.
Naye Meneja Masoko Taifa wa TDL, Joseph Chibehe alisema kinywaji hicho kitapatikana katika chupa zenye ujazo wa 750ml na Pakiti zenye ujazo wa 100ml, huku kikiuzwa kwa bei ambayo watu wengi wataimudu.
Chibehe alisisitiza kwamba kinywaji hicho kitapatikana kote nchini na watahakikisha kinapenya katika soko la Kimataifa, ili kuitangaza Tanzania juu ya vinywaji bora zaidi vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment