header

nmb

nmb

Tuesday, March 30, 2010

MSHIKAKI SI DAR PEKEE HATA MIKOAMINGINE!!

HILI NI KOSA AU SI KOSA.TUANDIKIE.BY GODWIN IR

TIMU YA JUDO YAKABIDHIWA JUKUMU LA BENDERA

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Nchini Idd Kipingu akimkabidhi Bendera ya Taifa Kapteni wa timu ya taifa ya Judo wakati chama cha judo nchini JATA kilipofanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea maadalizi yao na safari yao ya kwenda nchini Kenya katika jiji la Nairobi ambako mashindano ya kanda ya (5) baraza la Afrika katika mchezo wa judo yatayofanyika kuanzia 2-3 na baadaye yatafuatiwa na mazoezi ya pamoja kwa timu zote zitakazoshiriki katika mashindano hayo.
Timu inaondoka kesho alfajiri na inatarajiwa kurejea nchini tarehe 7/4/2010 na wachezaji wanaoondoka ni Omary Yusuf Ngowe, Andrew Thomas, Abuu Selemani, Athuman Abdalla na Zaidi Khamis (uzito wa kg60) wengine ni Fokas Mkude, Mohamed Korogombe, Philip Sabini (uzito kg66), Gervas Leonard, James Mapunda, Richard Martin (Uzito 73kg), Niclaus Mkinga, Gervas Taitas, Seif Malulu (Uzito81kg) na Eduward Nanda Mbambala (Uzito 90kg).
Wasichana ni Mary Francis, Latifa Mbezi (Uzito 63kg) na viongozi ni Kashinde Shaban Katibu Mkuu wa JATA na kocha wa timu hiyo Jose Valdes Silva na Hassan Mlilo Kiongozi wa Msafara, katika picha kushoto ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya judo Jose Valdes Silva.


MAZISHI YA ALIYEWAHI KUWA RPC MSAIDIZI KAMANDA SSP,MACHASSP ,MACHA AKIWA OFISINI ENZI ZA UHAI WAKE.KWA SASA ALIKUWA NI MSTAAFU

HISTORIA YA MAREHEMU HERI MACHA


WASIFU
Marehemu alizaliwa Tarehe 23/09 /1941 katika kijiji cha Kondeni.

ELIMU:
Alianza shule ya Msingi Kirua 1948 na baadaye alihamia Lutheran Middle School Lyakrim na kuhitimu darasa la Nane October 1956
1957 alijiunga na “AFRICA HIGH SCHOOL KYEBANDO – UGANDA” Ambapo alipata Certificate ya JUNIOR SECONDARY THREE LEAVING EXAMINATION.”

KAZI
1960 Aliajiriwa na kampuni ya ELEMENTARY TYPE WRITING hadi 1961, tarehe 11 / 1963 alijiunga na Chuo cha polisi (CCP) na kuhitimu kozi 01 / 06 / 1963 na kuanza kazi rasmi. 1967, katika mwaka huo alipandishwa cheo na kuwa ASSISTANT INSPECTOR nakudumu katika cheo hicho alidumu katika cheo hadi 1974 ,kutokana na Uadilifu wake mwaka huo huo alipandishwa cheo na kuwa FULL INSPECTOR akiwa Wilaya Korongwe mkoani Tanga.

Marehemu Macha alipandishwa cheo na kuwa SSP cheo alichodumunacho mpaka alipo staafu Jeshi 1997 akiwa Mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kustaafu Mzee Macha alirudi Kijijini kwake nakuendelea na shughuli za Kilimo hadi mauti ilipomkuta mwaka huu.
MAISHA YA NDOA
1963 marehemu alijaliwa kufunga ndoa n kupata watoto 6 watatu wakiwa wa kiume na watatu ni wakike .
KUUGUA. Na Mauti


Marehemu alianza kuugua Mwaka 1988 akiwa mkoani Tanga hali iliyopelekea afanyiwe upasuaji wa tumbo katika Hospitali ya Rufaa KCMC. Baada ya upasuaji huo Marehemu aliendelea kusumbuliwa na shinikizo la damu pamoja na ugonjwa wa Gout ambayo ilimfanya atibiwe katika hospital mbalimbali za Mkoa hadi mauti yalipomfika tarehe 24 / 03 / 2010, saa 5.30 usiku.

Marehemu ameacha Mjane, watoto 6 na wajukuu 8.

SHUKURANI:

Shukurani zetu za dhati ziwaendee Madaktari, manesi na wahudumu wote wa KCMC na hospitali zote za Mkoa ambazo Mzee aliwahi kutibiwa kwa lengo la kujaribu kuokoa uhai wake. Shukurani za pekee ziwaendee Mapadri / Wachungaji na wote waliotoa huduma za Kiroho, Pia wakwezake Mr Kaaya ,Mr Faki,na Mr Patrick,

Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa Kamanda Macha


Mke na Watoto wa Kiume wakiomboleza


Katika Majonzi mazito na huzuni kubwa ni mama yetu mke wa marehem Mrs Macha,kushoto. na watoto wake


Mtoto wa marehemu mama Sundey na mjukuu wa marehem Sundey wakiwa katika majonzi makubwa wakati wa kuaga mwili wa Mzee Macha

Baadhi ya ndugu na Jamaa kutoka mkoa wa Tanga ambako Mzee Macha aliwahi kufanya kazi wakiwa katika maombolezo.HAWA NI WAKWE WA MAREHEMU MACHA,KUTOKA KUSHOTO NI MR. FAKI NA MWANA prhabari.blogspot.com


Mtoto wa Marehem kulia. Merry Macha na Mjomba wa Marehem Stella G.Masue

Tumpambe Baba yetu Mungu amekupenda zaidi yetu

Sunday, March 28, 2010

UFUNGUZI WA BUNGE LA 122 LA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI MJINI BANGKOK!!

Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta akichangia katika mjadala kuhusu maswala ya kisiasa na kiuchumi Duniani wakati wa Mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika mjini Bangkok, Thailand, wikiendi hii.
Picha zote na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge
Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta, akifuatilia kwa makini ufunguzi rasmi wa mkutano wa 122 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ulioanza rasmi jana mjini Bangkok, Thailand kwa kufunguliwa na Mtoto wa Mfalme wa nchi hiyo, Princess Maha Chakri Sirindhorn . Walioketi kusho ni balozi wa Tanzania nchini Malaysia anayesimamia pia Thailand, Mhe. Cisco Mtiro, Mhe, Dkt Christine Ishengoma, Mhe. Idris Mtulia na Mhe. Suzan Lyimo.

MKUNGU WA NDINZI HUU UNAUZWA BUKU MBILI TU!!!

BINTI HUYU AKITEMBEZA MKUNGU WA NDIZI, ALIDAI KUWA MKUNGU HUU UUZWA BUKU MBILI TU. MKOANI KILIMANJARO KATIKA KIJIJI CHA KONDENI MARANGU
BODA HII UTUMIWA NA WAKAZI ZAIDI YA MIA TANO KWA SIKU

NIKIWA MOSHI MJINI KWA AJILI YA MAHITAJI YA KIJIJINI NILIKUTANA NA WANA PR WAANDISHI WA HABARI MKOANI KIRIMANJARO AMBAPO WALINIFARIJI


Kutoka kushoto Ni. Maleli Venans wa Kituo cha Radio ya Moshi FM, Zephania Renatus Mwakilishi wa Radio Free Afrika (RFA) Mie Katikati Mzee wa PR, Rodrick Makundi ambaye yuko mafunzoni katika Magazeti ya Uhuruu na Mazlendo, Pia kituo cha MOSHI FM. Wa mwisho ni Mkongwe KIJA ELIAS ambaye ni Mshika kamera wa kituo cha STAR TV

SHUKURANI ZA PEKEE ZIWAFIKIE WADAU WOTE WA PR HABARI KWA KUFANIKISHA MAZISHI YA BABA MKWE WANGU SSP MACHA KWA HALI NA MALI


MAREHEMU KAMANDA MSTAAFU WA JESHI LA POLISI MR. HERI MACHA AMEFARIKI DUNIA NYUMBANI KWAKE MOSHI KATIKA KIJIJI CHA KONDENI HIMO MKOANI KILIMAJARO MAZISHI YAKE NI KESHO.HABARI NA WASIFU WAKE NI BAADA YA YA MAZISHI.
TUKIWA UWANI KWA MAREHEMU MZEE MACHA KWA AJILI YA MAOMBOLEZO. MIE KAKA MZEE WA PR NA MKE WANGU MAMA H, KULIA KWANGU.WENGINE NI MASHEMEJI ZANGU NA WAKE ZAO

MAZEE HUKO MOSHI KITIZZZZ NI KAMA MBUZI KWANI NIKIWA KATIKA SAFARI YA KUELEKEA KATIKA KIJIJI CHA KONDENI NILIKUWA NIKIPISHANA NA KITIZZZZZ KAMA UONAVYO HAPA

LEO NI SIKUKUU YA MATAWI WA WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO

Dogo akikimbia kwa ajili ya kuvuka Barabara ya Mawenzi huku mkononi akiwa ameshika Tawi kuashiria sikukuu ya Matawi kwa Wakristo
Magari mengi ya mji wa moshi leo yanaonekana kupambwa na tawi moja moja.Pichani ni stendi Kuu ya Mabasi Mjini moshi leo
Friday, March 26, 2010

KILIMANJARO BIA WATANGAZA NOMINEES WA KILI MUSIC AWARDS 2010...


Mkurungenzi masoko wa TBL Bw. David Minja akiwa na meneja wa Kilimanjaro bia Bw. Georger Kavishe wakiwa katika mkutano wa kutangaza wasanii walio ingia katika vinyang'anyiro vya tunzo za Kili mwaka huu.

Wanaowania tunzo ya Mwimbaji bora wa kike.
Lady Jaydee
Mwasiti Almasi
Maunda Zorro
Vumilia Mwaipopo
Khadija yusuphu


Wanaowania tunzo ya Mwimbaji bora wa kiume
Marlow
Banana Zorro
Mzee Yusuphu

Ally Kiba

Christian Bella

Wanaowania Albamu Bora ya Taarab
Jahazi Modern Taarab (Daktari wa Mapenzi),
Five stars Modern Taarab (Riziki mwanzo wa chuki),
Coast Modern Taarab (Kukupenda isiwe tabu),
New Zanzibar star (Powa mpenzi),

East African Melody (Kila mtu kivyakevyake).


Tunzo ya Wimbo Bora wa Taarab inawaniwa na

Daktari wa mapenzi (Jahazi Modern Taarab),
Roho mbaya haijengi (Jahazi Modern Taarab),
Msitujadili na Riziki mwanzo wa chuki (zote Five stars Modern Taarab),

Kupenda isiwe tabu (Coast Modern Taarab).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Mwaka inawaniwa na

Marlow (pii pii - Missing my baby),
Diamond (Kamwambie),

Banana Zorro (zoba),
Hussein Machozi (Kwa ajili yako).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili kwa upande wa bendi ni
Machozi Band (Nilizama),
African Stars Band - 'Twanga pepeta' (Mwana Dar es salaam),
Top Band (Asha),
FM Academia (Vuta nikuvute),

Extra Bongo (Mjini Mipango).

Tunzo ya Albamu Bora ya Bendi inawaniwa na

African Stars Band - 'Twanga pepeta' (Mwana Dar es salaam),
Kalunde Band (Hilda),
Msondo Ngoma Music Band (Huna Shukrani).


Tunzo Bora ya Wimbo Bora wa R&B wanaowania ni
Belle 9 (Masogange),
Diamond (Kamwambie),
A.T na Stara Thomas (Nipigie),
Maunda Zorro (Mapenzi ya Wawili),
Steve (Sogea Karibu).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania inawaniwa na
Mrisho Mpoto (Nikipata Nauli),
Machozi Band (Mtarimbo),
Offside Trick (Samaki),
Wahapahapa Band (Chei Chei),

Omari Omari (Kupata Majaaliwa).

Wanaowania Tunzo Wimbo Bora wa Hip Hop ni

Joh Makini (Stimu Zimelipiwa),
Quick Racka (Bullet),

Chid Benz (Pom pom pisha),

Mangwea (CNN),

Fid Q (Iam a professional).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Reggae inawaniwa na

Hemed (Alcohol),
Dabo Ft. Mwasiti (Don't Let Go),
Man Snepa (Barua),
Matonya Ft. Christian Bella (Umoja ni Nguvu).

Kwa upande wa Wimbo Bora wa Ragga, wanaowania ni

Dully Sykes (Shikide),
Bwana Misosi (Mungu yupo bize),
Drezzy Chief (Wasanii),
Benjamin wa mambo jambo (Fly).


Tunzo ya Rappa Bora wa Mwaka inawaniwa na

Chokoraa
Ferguson
Kitokololo

Totoo ze bingwa

Diouf

Tunzo ya Msanii Bora wa Hip Hop ni
Joh Makini
Chid Benz
Mangwea

Profesa jay

Tunzo ya Wimbo Bora wa Africa Mashariki inawaniwa na

Blue 3 Ft. Radio and Weasal (Where you are),
Kidum Ft. Juliana (Hturudi nyuma),

Cindy (Na Wewe),
Radio and Weasal (Bread and Butter),
Kidum (Umenikosea).

Tunzo ya Mtunzi Bora wa nyimbo ni

Mzee Yusuphu
Mrisho Mpoto
Lady Jyadee
Banana Zorro


Tunzo ya Mtayarishaji Bora wa Muziki ni

Lamar Marco Chali
Hermy B

Allan Mapigo

Man Water

Video Bora ya Muziki wa Mwaka inawaniwa na
Lady Jaydee (Natamani kuwa Malaika),
Diamond (Kamwambie),
AY (Leo),
Banana Zorro (Zoba),
C Pwaa (Problem).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Fro Pop inawaniwa na


Banana Zorro (Zoba),
Ally Kiba (Msiniseme),
Marlow (Pii pii - Missing my baby),
Mataluma (Mama Mubaya),

Chegge (Karibu kiumeni).


Tunzo ya Msanii Anayechipukia

Belle 9
Diamond
Barnaba

Quick Racka
Amini

Tunzo ya Wimbo Bora wa Kushirikiana unawaniwa na

AT na Stara Thomas (Nipigie),
Mangwea na Fid Q (CNN),

Barnaba na Pipi (Njia Panda),
Mwana FA na Profesa Jay na Sugu (Nazeeka Sasa),
Hussein Machozi na Joh Makini (Utaipenda).

Thursday, March 25, 2010

Rubani feki hadi mamtoni wakwea mapipa mnasikia hii!!


Wakati hapa Tanzania kumekuwa na gumzo la kuhusu kuwepo wa wataalamu na wanaowanatumia vyeti feki, halia kama hiyo pia iko katika bara la Ulaya.


Rubani wa Uswisi aliyekuwa na leseni feki amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Amsterdam, wakati akijiandaa kurusha ndege yenye abiria 101 aina ya Boeing 737 kuelekea Uturuki, polisi wa Uholanzi walisema.


Mtu huyo mwenye umri wa miaka41 ambaye ni mswideni, alikwua akifanya kazi Ankara, amekuwa akirusha ndege kwa miaka 13 akiwa amekaa ngani kwa zaidi ya saa 10,000 alikwua akitumi vyeti feki kwa ajili ya kurusha ndege Ubelgiji, Uingereza na Italia, Polisi ilisema.
Rubani huyo ambaye jina lake halikutajwa, alishindwa kujieleza vizuri wakati alipokamatwa na kuvuliwa magwanda ya urubani.

Breking Newzzzzzzzzzzzz Lori laangukia kipanya lauwa abiria wote 10 KibambaHii ni changa moto kwa kamanda mpya Kaka MpingaLukasi akitoa Maelezo jinsi alivyo piga picha hizo ambazo kweli ukiziona zina sisimuwa na kusikitisha sana

Mpiga Picha Lukasi wa BTL akiwaonyesha Picha za Miili ya walio Aga Dunia leo asubu


Kompyuta ikionesha mmoja ya picha zilizopigwa na bw. Lukasi.Picha hiyo inaonyesha Roli likiwa kipanya hicho kiasi .Baadhi wametolewa vipande


MUNGU ZIWEKE ROHO ZA MAREHEM PEPONI. prhabari kwa wote Pia inaungana na Ndugu na jamaa wa Marehemu katika kipindi hiki kizito cha Msiba

ABIRIA zaidi ya 11 wamekufa papo hapo katika ajali mbaya ya barabarani baada ya lori la mafuta lenye tela kugonga na kuiburuza mtaroni kisha kukandamiza daladala aina ya kipanya katika barabara ya Morogoro eneo Kibamba, Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi ya Dar es Salaam, Bw. Elias Kalinga akizungumza ilipotokea ajali hiyo eneo la Kwa Mangi, Kibamba jana alisema idadi kamili ya maiti waliokufa katika ajali hiyo huenda ikaongezeka baada ya miili ya marehemu hao kukatika vipande vipande.


"Mpaka sasa inadadi ya maiti ni 11 lakini idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu miili imekatwa katwa na kutenganishwa viongo vya mwili"alisema Kamanda Kalinga.


Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri wakati lori lililokuwa limebeba mafuta ya taa aina ya FIAT IVECO T186 ABP likiwa na tela T 192 ABP mali ya Kampuni ya Mahmod Mohamed Duale Transporter likitokea Dar es Salaam kwenda Isaka, Shinyanga kugonga Hiace iliyokuwa ikitoka Kongowe, Kibaha kwenda Ubungo Dar es Salaam.


Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa lori hilo lilivuka kutoka upande wake kwenda upande wa pili wa barabara na kugonga kipanya T615 AJW ambacho kukiburuza kwa umbali wa mita kadhaa kabla ya kukandamiza mtaroni kufanana na chapati.


Katika eneo la ajali, kazi ilikuwa ngumu iliyotumia takribani saa kumi kunasua miili ya watu waliokandamizwa na lori hilo kutokana na kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kunyanyua uzito mkubwa.


Wakati wengine wakitafuta njia ya kunasua miili hiyo wakazi wengine wa eneo hilo walivamia eneo hilo wakiwa na ndoo za kuchota mafuta yalikuwa wanamwagika baada ya kutoa tenki la mafuta.


Askari wa jeshi la Polisi waliokuwepo kusaidia ulinzi, walifanya kazi ya ziada kuzuia watu kusogea eneo hilo hadi saa 7 mchana kazi ya kupakua mafua ilipofanyika na lori hilo kunyanyuliwa kunasua matiti waliokuwa wamekandamizwa.


"Tumezuia watu wasisogee eneo la ajali kwa sababu Walishatoboa tenki na kukinga mafuta,lakini matundu yamezibwa na limekuja tenki jingine kupakua mafuta ili uzito upungue winchi linyanyue lori hilo ili maiti wanasuliwe" alisema polisi mmoja ambaye hakutaja jina.


Katika jitihada za awali waokoaji, Kikosi cha Zimamoto cha Halamshauri ya Jiji la Dar es Salaam na wasamaria walifanikiwa kunasua maiti wawili ambao walipelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha.


Msemaji wa hospitali ya Tumbi, Bw. Gerald Chami alisema maiti mmoja imetambuliwa kuwa ni kondakta wa daladala hilo,Shukuru Mhagile (28) mkazi wa Kibamba CCM na msichana mmoja ambaye hajatambuliwa aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24-26.


Inadaiwa kuwa dereva wa lori la mafuta alikuwa amesinzia na gari hilo kuhama kutoka upande wake na kwenda kugonga kipanya hicho na kukandamiza watu waliokuwemo katika daladala hiyo.


Wananchi waliofurika eneo la tukio hilo walilalamkia Serikali kutokuwa na vifaa vya kisasa vya uokoaji na kusababisha kuchelewa kufika eneo la tukio.


"Hii kazi ya kunasua miili ya marehemu hawa ingeokoa maisha ya wale waliokuwa wamepata majeraha makubwa lakini walikuwa bado hai, ajali imetokea saa 11 alfajiri waokoaji wanakuja saa nne hata majeruhi watakuwa wamekufa" alisema mkazi mmoja ambaye alikataa kusema jina lake.


Kamanda Kalinga alisema atatoa taarifa nyingine ya ajali hiyo baadaye, maiti wamepelekwa hospitali ya Tumbi na wengine hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa.


Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya CHADEMA, Bw. John Mnyika ametuma salamu za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki na wafiwa wote kufuatia ajali mbaya iliyotokea jana asubuhi Kibamba jijini Dar es Salaam.


Bw. Mnyika alisema CHADEMa inatoa mwito kwa Serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vyanzo vya ajali za mara kwa mara katika eneo la Kibamba ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Alisema ikumbukwe kuwa Desemba mwaka 2007 ajali nyingine ilitokea eneo la hospitali ya Kibamba ikihusisha malori na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo mjamzito na wengine 11 kujeruhiwa.

Alisema Aprili mwaka 2008 bunge liliarifiwa kuwa jumla ya watu 181 wamepoteza maisha kwa kugongwa na magari kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2007 katika eneo la kuanzia Kibamba mpaka Ubungo kwenye mataa.

Alisema Mei 2009 madereva wawili walikufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso huko maeneo hayo hayo ya Kibamba na Januari 2010 watu 18 walijeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Morogoro eneo la Kibamba Darajani ambapo magari matano yaligongana kwa pamoja.

Wednesday, March 24, 2010

MAMBO YA MISS TANZANIA


Baadhi ya Mawakala wa Mashindano ya Urembo Nchini, wakiwa katika semina elekezi Dar es salaam jana .kutoka kushoto ni Borah Lemmy ,Doracia Kayombo, Mariam Amiry na Ciana Swai Pix.Rajabu

UZINDUZI WA UZAZI WA MPANGO. ULIVYO FANA

MC. MWALEKWA
Hotuba ya Mr. Daniel Crapper

Speech for Daniel

Hon. Deputy Minister for Health & Social Welfare, Dr. Aisha Kigoda,
Asst. Director for Reproductive Health & Maternal Child,Dr. Neema Rusibamayila
Ilala Deputy Mayor, Hon. Jerry Slaa
Mchafukoge Ward Councilor, Hon. Yakoub
Members of UN agencies present
MoHSW members present
PSI partners and staff members present

Ladies and Gentlemen, good-morning and welcome!

It is a pleasure to meet all of you today to talk about reproductive health issues. As you know, Tanzania has achieved good success in HIV/AIDS and malaria over the past few years, and the rate of new HIV infections is going down, as is the number of deaths caused by malaria.

This is not the case for family planning: many men and women in Tanzania are still in need of family planning products and services and are not able to find the method that suits them best.

On one hand, choosing to plan your family can be considered a very personal choice, but on the other hand, it is really important to remember that family planning is a key strategy to reduce maternal mortality, to improve the health of mothers and newborn babies, and to allow families to take better care of their children.

The government of Tanzania recognizes the importance of family planning and is demonstrating its commitment to make services widely available throughout the country. By 2015, the GoT would like to see 60% of couples using a method to plan their families. But today as we speak, the level of use is still low, below 25% of the population (of reproductive age), even though another 25% claim that they would like to space or limit their family but are not using any method.

One of the key barriers to achieving a higher rate of use in Tanzania remains misconceptions: people have misconceptions about what family planning is about (some say it is an invention by white people to limit the population in Africa); there are misconceptions about how modern contraceptives work (some people think it can cause cancer or make women infertile); and there are misconceptions about what to expect when using modern family planning methods (can a baby really be born with an IUD in its hand??).

There is also a lack of involvement from men as key decision-makers in health issues, as well as a lack of understanding about how these methods work, how safe they are, and how highly effective they are.

This past year, PSI Tanzania has been in contact with thousands of men and women in the field and has listened to their questions, their experiences, their fears. In some remote areas around Mwanza, PSI teams were greeted by women saying “where have you been all these years? Why are you coming only now? I have 11 children and I want no more”.

From this research, and other quantitative and qualitative research, PSI Tanzania was able to identify key messages that need to be communicated to help men and women adopt a healthier behavior and better plan their families: these are messages about choice, messages about achieving their aspirations and their goals through better planning, and messages about the safety, the effectiveness and the ease of use of contraceptive methods.

The campaign starting today will be rolled out at various levels. Mass media messages through the Amka radio drama and newspapers strips will definitely raise awareness and create interest; but they will also be strongly supported by on-the-ground interventions in local communities. In partnership with local government authorities, PSI will increase its efforts in IPC activities, involving men and women at the community level, and linking them to trained providers in the field to guarantee access to better counseling, better choice of methods, including long-term methods, and high quality services.

As we are about to unveil the core concept of the campaign, it is important for us to thank the key contributors to this campaign: first, the Ministry of Health and Social Welfare in particular the IEC unit and Health Education Unit for their constant guidance and support; all our partners present today without forgetting the media who will contribute to make this campaign a success.

With these words, I would like to welcome you again and I hope you enjoy this event.
Thank


Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.Asha Kigoda(kulia) akipokea mchoro wa picha yenye sura yake huku ikiwa imepambwa na rangi za Uzazi wa Mpango huo, kutoka kwa Mkurugenzi wa mawasiliano wa shirika la PSI Bi.Mery Mwanjelwa.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Mchafukoge Bw. Mohamed Yakybu,Mkurugenzi wa PSI Tanzania,Bw.Daniel Crapper na Naibu Mkurugenzi wa PSI,Bw.Romanus Mtung'e


MPOTO


Taarifa kwa Vyombo vya Habari
PSI Tanzania yazindua kampeni kuhamasisha matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango

Kwa maelezo zaidi
Wasiliana na Mary Mwanjelwa
Mkurungenzi wa Ushirikiano
PSI/Tanzania
Simu: 0787 032800
Barua pepe:
mmwanjelwa@psi.or.tz

Dar es Salaam Machi 24, 2010 … Katika kuendeleza juhudi za kuhamasisha matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango na kuondoa dhana potofu kuhusiana na huduma hizo, shirika la PSI/Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo limenzidua kampeni ya kitaifa itakayolenga maeno hayo.Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuelimisha umma na kutoa taarifa sahihi kuhusiana na matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango, njia zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango na faida zitokanazo na uzazi wa mpango.
Ili kuhakikisha kuwa taarifa sahihi zinawafikia wananchi wote hapa nchini, PSI/Tanzania imepanga kutumia njia zote kuu za mawasiliano, radio, luninga, magazeti, michezo ya kuigiza, mabango ya matangazo na michoro katika maeno mbalimbali hapa nchini.Akiongea katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Aisha Kigoda alisema inasikitisha kuona kwamba bado Watanzania walio wengi wahawatumii njia za kisasa za uzazi wa mpango wakati huduma hizo zipo.Alisema pamoja na jitihada nyingi ambazo zinafanyika za uhamasishaji wa matumizi ya uzazi wa mpango bado matumizi ya njia hizo hapa nchini yapo chini.
“Takwimu zinaonesha kwamba ni asilimia 20 tu ya walengwa waliotarajiwa kutumia ndio wanaotumia njia za kisasa katika kupanga uzazi.“Idadi hii ni ndogo sana na hasa ikizingatiwa kuwa bado wananchi walio wengi wanaendelea kupata watoto bila kupanga na wengi wao wanashindwa hata kuwapatia huduma muhimu za kijamii. Idadi kubwa ya watoto pia inakuwa mzigo kwa wanajamii husika na serikali yetu,” alisema Waziri.Alisema kuwa pamoja na idadi ya watumiaji wa njia za uzazi wa mpango kuwa ndogo, pia taifa linakabiliwa na tatizo lingine la kuwa na idadi kubwa ya wanawake ambao hawajifungui kwa wakati muafaka. Wanawake walio wengi hapa nchini wanajifungua ama mapema sana, yaani wakiwa na umri mdogo au wakiwa wamechelewa, yaani wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 35.“Takwimu zinatuonesha kwamba akinamama wengi hapa nchini wanapoteza maisha kwa sababu ya kubeba ujauzito katika muda ambao sio muafaka. Ama wanabeba ujauzito wakiwa na umri mdogo sana, ama wakiwa na umri mkubwa sana au wanabeba ujauzito mara nyingi sana na wengine wanabeba ujauzito mara kwa mara, yote haya ni hatari kwa maisha ya akinamama,” alisema Dk Aisha.Alisema kutokana na sababu hizo akina mama wengi wanapoteza maisha wakati wa kujifungua na kuacha watoto wao ambao baadhi yao hupoteza maisha kutokana na kukosa malezi bora.Waziri aliongeza kusema kwamba serikali inachukua juhudi za makusudi katika kushughulikia matatizo ya vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua. Alisema kuwa hivi sasa juhudi zinafanywa katika kuboresha huduma katika wodi za kujifungulia na uhamasishaji wa wajawazito kuhakikisha wanajifungua katika vituo vya afya ili kupata msaada wa wauguzi.Alisema kuwa serikali imejiwekea malengo ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2015 idadi ya watumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango inaongezeka hadi kufikia asilimia 60.Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa PSI, Daniel Crapper, alisema yapo mambo mengi yasiyo ya kweli yanayozungumzwa mitaani kuhusiana na njia za kisasa za uzazi wa mpango.Alisema zipo huduma za aina nyingi za uzazi wa mpango na kwamba katika hizo kila mwanamke anaweza kupata aina mojawapo ambayo anaweza kutumia bila kupata madhara yoyote ya kiafya.“Ni vema wanannchi wakaelewa kwamba njia za kisasa za uzazi wa mpango ni salama kiafya na zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na idara nyinginezo za serikali,” alisema Crapper.Aliongeza kusema kuwa mambo mengi yanayozungumzwa mitaani kuhusiana na athari za njia za kisasa za uzazi wa mpango ni za uzushi na kushauri wananchi kupata ushauri wa watoa huduma za uzazi wa mpango kabla ya kuanza kutumia njia hizo.


VIJANA HAWA WANA FANYA NINI

WAUCHAPA USINGIZI HADHARANI. Kweupeee nje ya ofisi yao mida hii

katuni yetu na Nathan .Ni jukumu letu sote kutetea Wafafunzi


Tuesday, March 23, 2010

JAMAA NINOMA


WLADIMIR KLITSCHKO insists it will be a 'pizza' cake IF he climbs into the ring with David Haye.


Klitschko successfully defended his WBO and IBF world heavyweight titles with a sensational last-round knockout of Eddie Chambers in Dusseldorf.


WBA king Haye pulled out of one showdown with Wladimir last year, citing a back problem that flared up a week before the fight was due to take place.


His withdrawal incensed the 33-year-old Ukrainian - who suspected Haye did not want to fight.
And, after destroying American Chambers with a vicious left-hook, he raged: "I will do the same to Haye if I get him.


"His face will be really messed up and look like a pizza when I have finished with him.
"He is criticising me as nothing more than jab, jab, grab. Ask Chambers about that will you?
"Like I knocked out Chambers, I will knock out Haye. He will be the 49th knockout on my record."


Haye defends his version of the world title against Johnny Ruiz in Manchester on April 3 - and he wants to unify the division by taking on Wladimir and his brother Vitali Klitschko before retiring.


Klitschko admitted he is not fully convinced Haye's back injury was genuine and he added: "Actions speak louder than words.


"He bitched out twice - me and then my brother Vitali.


"Maybe there was an injury but twice in a row makes me suspicious.


"He bailed out against both of us.


"Fans in Britain would love to see this fight. He should give his own fans respect and face me.
"I am upset with many things concerning David Haye.

MAMBO YA MAHAKA ZETU LEO


Veronica Ikonga na Irene Mpatwa, Dar leo

MKAZI mmoja wa Buguruni Kisiwani, Ramadhani Juma (29), amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni kujibu mashitaka ya kuvunja nyumba.

Mshitakiwa huyo amesomewa shitaka lake na karani Vicky Mroso mbele ya hakimu Jamirah Ramadhani katika mahakama hiyo.

Imedaiwa kuwa Machi 13, mwaka huu, saa 7 mchana, mshitakiwa huyo alivunja nyumba ya mlalamikaji Shija Jongo kwa nia ya kutenda kosa.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo baada ya kuvunja nyumba alichukua simu ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya sh. 80,000, mkoba wenye thamani ya sh. 120,000 na fedha taslimu sh. 30,000.

Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na kesi yake itatajwa tena Machi 29, mwaka huu.

Katika kesi nyingine, mkazi wa Buguruni Kisiwani, Salum Said (48), amefikishwa kizimbani hapo kujibu mashitaka ya kutoweka na fedha za luku mali ya mlalamikaji Haji Zuberi.

Imedaiwa kuwa Septemba 25, 2009, Vingunguti Wilaya Ilala, mshitakiwa alikimbia na fedha hizo baada ya kupewa kwenda kununulia umeme wa LUKU.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi yake itatajwa tena Machi 29, mwaka huu.