header

nmb

nmb

Tuesday, March 23, 2010

MAMBO YA MAHAKA ZETU LEO


Veronica Ikonga na Irene Mpatwa, Dar leo

MKAZI mmoja wa Buguruni Kisiwani, Ramadhani Juma (29), amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni kujibu mashitaka ya kuvunja nyumba.

Mshitakiwa huyo amesomewa shitaka lake na karani Vicky Mroso mbele ya hakimu Jamirah Ramadhani katika mahakama hiyo.

Imedaiwa kuwa Machi 13, mwaka huu, saa 7 mchana, mshitakiwa huyo alivunja nyumba ya mlalamikaji Shija Jongo kwa nia ya kutenda kosa.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo baada ya kuvunja nyumba alichukua simu ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya sh. 80,000, mkoba wenye thamani ya sh. 120,000 na fedha taslimu sh. 30,000.

Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na kesi yake itatajwa tena Machi 29, mwaka huu.

Katika kesi nyingine, mkazi wa Buguruni Kisiwani, Salum Said (48), amefikishwa kizimbani hapo kujibu mashitaka ya kutoweka na fedha za luku mali ya mlalamikaji Haji Zuberi.

Imedaiwa kuwa Septemba 25, 2009, Vingunguti Wilaya Ilala, mshitakiwa alikimbia na fedha hizo baada ya kupewa kwenda kununulia umeme wa LUKU.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi yake itatajwa tena Machi 29, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment