header

nmb

nmb

Wednesday, January 20, 2010

Wazazi wa MBOZI chanzo cha mimba kwa wanafunzi Mbeya!


(source; Esther Macha wa Mbozi)

ONGEZEKO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya, imeleezwa kuwa chanzo kikuu ni wazazi wa watoto hao kuwaficha wanaume wanaowapa mimba kwa kuwapatia zawadi ili wasiwapeleke kwenye vyombo vya sheria,

imeleezwa kuwa tatizo la mimba kwa wanafunzi limekuwa likiongozeka kila siku kwa wilaya mbozi na tatizo hilo kuchangiwa na wazazi wenyewe kwa kuwa na tamaa ya kupokea vizawadi kutoka kwa wanaume waliowapa mimba watoto wao wakishirikiana na wazazi wa wanaume wanaowapa mimba.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Mkoani Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoani hapa Bi.Frolence Kyendesya wakati alipofanya ziara ya kuzuyngumza na wanawake wa Wilaya tano za Mkoa wa Mbeya kuhusiana na tatizo la mimba kwa watoto kike ambalo limekuwa ni kero kubwa kwa wilaya hiyo.

Bi. Kyendesya alisema ifike wakati kwa wazazi kuwa mstari wa mbele kukemea suala la mimba kwa watoto na tabia iliyojengeka miongoni mwao ya kuwa na tamaa ya kupokea vizawadi kwa wanaume wanaowachafua watoto wao ife mara moja na badala yake wajali elimu kwa mtoto wa kike.

"Kwa kweli katika kuwaficha wanaume hawa mzazi mara baada ya kupokea zawadi hizo humwita mwanae na kumwambia kuwa kama akiulizwa na mtu yeyote kuhusu mimba aseme kuwa alipata mnadani na asimtaje mwanaume yeyote akatae kabisa hata akipelekwa mahakamani , sasa hili jamani hebu wazazi wenzangu tuliache basi tuwe na huruma na watoto wetu hawa ni taifa la kesho"alisema Mwenyekiti huyo.



Aidha alisema kuwa watoto wengine ni wadogo kiasi kwamba hawana uwezo wa kusukuma mtoto , kama wazazi wanatakiwa kuacha tamaa ya kupokea zawadi .

Aliendelea kusema kuwa wazazi wanapaswa kuanzia sasa kuanza kuomboleza kwa kuwafichua wale wanaowapa mimba watoto wao na wawe na uchungu wa kufanya hivyo kwani wanawake ndio wanaoteseka kwa suala la mimba za watoto .

No comments:

Post a Comment